Home Soka Simba sc Warejea Kambini

Simba sc Warejea Kambini

by Sports Leo
0 comments

Mastaa wa klabu ya Simba sc wamerejea kambini tayari kwa maandalizi ya kujiandaa na michuano ya kimataifa ambapo wanatarajiwa kuwavaa Asec Mimosa siku ya Novemba 25 itakayofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Idadi ya wachezaji wengi waliohudhuria mazoezi hayo wengi ni wale ambao hawajaitwa katika timu zao za taifa na wameingia moja kwa moja katika mazoezi ya gym kwa ajili ya kurejesha utimamu wa mwili.

“Wengi wamerudi leo kwa ajili ya mazoezi ya gym ambayo yamefanyika katika hosteli zetu zilizopo mbweni jijini Dar es salaam tayari kujiandaa kwa ajili ya michuano ya kimataifa ambapo tutawavaa Asec Mimosa katika dimba la Benjamini Mkapa”Alisema Ahmed Ally Meneja habari wa klabu ya Simba sc.

banner

Timu hiyo mbali na kurejea mazoezini pia ipo katika mchakato wa kumtafuta kocha mpya kwa ajili ya kuifundisha klabu hiyo baada ya kuachana na kocha Roberto Oliveira ambapo kwa mujibu wa Meneja wa Habari wa klabu hiyo ni kwamba wiki hii kocha huyo atatambulishwa rasmi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited