Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuibuka na alama tatu muhimu katika mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate uliofanyika katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es salaam baada ya kuifunga tiimu hiyo mabao 3-1 na kuendelea kuipambania nafasi ya kuchukua ubingwa wa kombe la ligi kuu nchini.
Iliwachukua Simba sc dakika nane pekee kupata mabao mawili ya harakaharaka yaliyofungwa na Saido Ntibanzokiza aliyekua mwiba mchungu kwa Singida Fg katika mchezo huo ambapo alifunga bao la kwanza dakika ya sita ya mchezo baada ya mabeki wa Singida kuzembea kuokoa mpira uliozagaa ndani ya boksi la hatari kufuatia kipa Benjamini Haule kupangua shuti kali la Cletous Chama huku akifunga bao la pili kwa penati baada ya beki Laurean Makame kuunawa mpira.
Simba sc ilifanikiwa kupata bao la tatu baada ya mshambuliaji Fredy Michael kufanya kazi ya ziada kuwatoka walinzi wa klabu ya Singida Fg na kupiga shuti ambalo liligongwa na beki na kumpita kipa Benjamini Haule na kumawamaliza kabisa Singida Fg ambao hawakua na la kufanya.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Saido sasa anafikisha mabao saba katika ligi kuu msimu huu huku klabu yake ya Simba sc ikifikisha alama 42 katika michezo 18 ya ligi kuu ambapo sasa wamezidiwa alama nane na vinara wa ligi kuu ya Nbc Yanga sc.