Timu ya Simba sc kesho itasafiri kwenda kanda ya ziwa kucheza na Kagera sugar na Biashara united ya mkoani Mara katika michezo ya ligi kuu Tanzania bara.
Simba sc itasafiri kinyonge kwenda mkoani Kagera kucheza na wababe hao ambao waliwafunga mechi zote mbili za ligi msimu uliopita baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 mjini bukoba na 1-0 hapa Dar es salaam.
Mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania bara kwa mara mbili mfululizo watasafiri bila nahodha John Boko ambaye ni majeruhi huku pia Cletous Chama na Gadiel Michael nao wakiripotiwa kuikosa michezo hiyo kutokana na majeruhi huku Erasto Nyoni akiwa na matatizo binafsi japo haijathibitishwa rasmi kukosa mchezo huo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba tayari imecheza michezo miwili ya ligi kuu ikifanikiwa kuweka kibindoni pointi zote sita baada ya kuwafunga Jkt Tanzania pamoja na Mtibwa sugar.