Home Soka Simba,Okwi Wafikia Patamu

Simba,Okwi Wafikia Patamu

by Sports Leo
0 comments

Ile inshu ya kuongeza mkataba ya staa wa Simba Emmanuel Okwi ni kama inaelekea mwishoni baada ya staa huyo kukubaliana baadhi ya vipengele na vigogo wa Simba walioko nchini Misri kuisapoti timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars).

Mganda huyo hapo awali aligoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo huku akionyesha viasharia vya kutaka kuondoka klabuni hapo huku taarifa zikidai timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika ya kusini inammendea staa huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi tofautitofauti za ushambuliaji.

”Okwi ameonesha nia ya kuendelea kusalia na sisi baada ya kufanya mazungumzo naye hapa misri hivyo tunatumaini kama hatobadili msimamo wake basi atasaini hivi karibuni”kilisema chanzo chetu cha habari.

banner

Okwi amekua mchezaji muhimu kwa mabingwa hao mara mbili mfululizo wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu akishirikiana na Meddie Kagere  na John Boko.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited