Winga wa zamani wa klabu ya Simba Ramadhani Singano “Messi”amejiunga na klabu ya Tp Mazembe ya nchini Kongo baada ya kumaliza mkataba na Timu ya Azam fc.
Singano alijiunga na Azam fc akitokea Simba sc baada ya kuwa na mgogoro wa kimkataba na klabu hiyo hali iliyowalazimu shirikisho la soka (Tff) kuingilia kati na kuamua mgogoro huo kwa mchezaji kuwa huru.
Pia winga huyo alishafanya majaribio katika klabu ya Diffaa El-Jadid ya nchini Moroko miaka miwili iliyopita japo walishindwana vipengele vya mkataba na maslahi.