Home Soka Sonso Wala Hana Noma

Sonso Wala Hana Noma

by Sports Leo
0 comments

Beki wa Yanga Ally Mtoni Sonso ameamua kufunguka baada ya kutemwa katika kikosi cha taifa stars kinachojiandaa na mechi ya michuano ya mataifa ya afrika kwa wachezaji wa ndani(Chan) dhidi ya kenya mchezo utakaopigwa julai 28 mwaka huu.

Baada ya kikosi hicho kutangazwa na kocha Ettiene Ndayiragije na jina la staa huyo aliyesajiliwa na Yanga akitokea Lipuli Fc ya Iringa amesema kuwa hana tatizo na kikosi hicho kwani lengo ni moja tu kutetea bendera ya taifa la Tanzania.

Pia staa huyo amekanusha kuhusu kuwa na kinyongo na kocha Ndayiragije kwa kuheshimu uteuzi wa kocha huyo aliyeibukia mbao kabla ya kuja Kmc na sasa ni kocha wa Azam fc.

banner

Sonso ni moja ya mabeki waliofanya vizuri msimu uliopita akiiongoza Lipuli Fc kufika fainali ya kombe la shirikisho japo walipoteza mbele ya Azam Fc na sasa amesajiliwa na Yanga sc na tayari ameshajiunga na kambi ya timu hiyo mkoani Morogoro baada ya kuwa na mapumziko mafupi baada ya kutoka katika michuano ya Afcon.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited