Mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa Sportpesa Tanzania Abbas Tarimba amesema mwaka huu (2020) hakutakuwa na Mashindano ya Sportpesa kutokana na kuyumba kwa uchumi wa kampuni hiyo kulikotokana na mlipuko wa Corona.
Pia Mkurugenzi huyo amebainisha hawana uhakika kama wataongeza mikataba mipya ya udhamini katika klabu za Simba sc, Yanga sc na Namungo sababu ikiwa ni kuyumba kwa uchumi kwa kampuni hiyo sababu ya Corona.
Ikumbukwe nchini Kenya kampuni hiyo ilijitoa kudhamini baadhi ya klabu ikiwemo klabu bingwa mara (19) ya ligi ya Kenya Gormahia na kusababisha kuyumba vibaya kwa uchumi wa vilabu hivyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.