Home Soka Stars,Sudan Hapatoshi Kesho

Stars,Sudan Hapatoshi Kesho

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa stars) kesho itashuka uwanjani kupambana na Sudan katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya afrika kwa wachezaji wa ndani zitakazofanyika nchini Cameroon mwaka 2020.

Mchezo huo utafanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam huku katika maandalizi ya mchezo huo kocha wa stars aliita wachezaji 25 huku akiwaacha makipa tegemeo wa Simba sc Aishi Manula na Benno Kakolanya.

Stars ikishinda mchezo huo itajiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali hizo ikizingatiwa mchezo wa marudiano unaweza kufanyika nchini Rwanda kufuatia hali ya usalama nchini Sudan kutotengemaa.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited