Home Soka Vipigo Vyazua Balaa Man Utd

Vipigo Vyazua Balaa Man Utd

by Sports Leo
0 comments

Kufanya vibaya kwa klabu ya manchester united ndani ya uwanja kumeanza kuleta balaa baada ya mdhamini mkuu wa jezi za klabu hiyo kampuni ya magari ya General motor ambayo kupitia nembo ya magari ya Chevrolet imegoma kuongeza mkataba na klabu hiyo pindi utakapoisha msimu ujao.

Fununu zinadai mgomo unasababishwa na matokeo mabaya ya united tangu kampuni hiyo ianze kuidhamini klabu hiyo huku kukiwa hakuna dalili za kuchukua mataji hasa ya ligi kuu na kombe la klabu bingwa barani ulaya kwa siku za karibuni.

Klabu hiyo iliingia mkataba wa miaka saba kwa dau la rekodi la kiasi cha paundi milioni 450 mkataba ambao utaisha katika msimu wa 2020/2021 na tayari united imeanza mchakato wa kutafuta mdhamini mwingine wa jezi.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited