Inaelezwa klabu moja kutoka huko Arabuni inajipanga kuleta ofa Jangwani baada ya kuvutiwa na uwezo wa winga Bernard Morrison aliyesajiliwa na klabu hiyo mwezi Januari mwaka huu
Klabu hiyo inayomilikiwa na matajiri wa mafuta, imeandaa kitita cha zaidi ya Tsh Milioni 900 kwa ajili ya kumnasa nyota huyo ambapo dau hilo ni maalumu kwa ajili ya kuvunja mkataba wa miaka miwili wa nyota huyo aliousaini msimu huu.
Taarifa tuliopata Morrison ameandaliwa mshahara wa Tsh Milioni 17 kwa mwezi pesa ambayo waarabu hao wanaamini inatosha kabisa kumshawishi winga huyo kuhama Jangwani.
Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaelezwa kuwa klabu hiyo inasubiri barua rasmi ili kuijadili na kutoa uamuzi kuhusu kufanyika kwa biashara hiyo.