Home Soka Winga DRC Atua Singida FG

Winga DRC Atua Singida FG

by Sports Leo
0 comments

Winga wa klabu ya Fc Lupopo Manu Labota Bola ameamua kujiunga na Singida Fountain Gate Fc na kuikacha ofa ya Yanga sc na tayari dili hilo limeshakamilika ukisubiriwa utambulisho tu klabuni hapo.

Awali Yanga sc ndio ilikua ya kwanza kuonyesha nia ya kumsajili winga huyo lakini ilianza kusuasua kukamilisha usajili huo ndipo mabosi wa Singida Fg walipoamua kumpandia ndege mpaka nchini Congo Drc na kukamilisha usajili huo haraka.

Mabosi wa Singida Fg pamoja na kukamilisha dili hilo iliwalazimu kufanya kazi ya ziada ili kuvunja mkataba wa staa huyo ambapo walifanikiwa baada ya kuzungumza na tajiri wa klabu hiyo  Jacques Kyabula Katwe ambaye pia ni gavana wa jiji hilo ambapo zaidi ya Tsh 250 milioni zilitumika kukamilisha dili hilo.

banner

Singida Fg ipo katika maboresho makubwa ya kikosi chake msimu huu ambapo pamoja na kusajili usajili wa maana dirisha kubwa sasa inafanya maboresho machache katika dirisha dogo la usajili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited