Mchezaji wa zamani wa FC Barcelona Xavi Hernandes ndiye kocha anayetajwa kuwa karibu zaidi kurejea katika timu hiyo na kuwa mkufunzi mkuu baada ya kufukuzwa kwa Ronald Koeman usiku wa Jumatano.
Koeman aliyekuwa akihusishwa kufutwa kazi kwa muda mrefu,hatimaye amefukuzwa baada ya kichapo cha 1-0 kwenye La liga dhidi ya Rayo Vallecano.
Xavi kwa kwasasa ni kocha mkuu wa klabu ya Al Saad ya Saudia Arabia,mazungumzo ya kusitisha mkataba wake yanaendelea leo Alhamisi kati ya Barcelona,Al Saad na Xavi mwenyewe na huenda akatangazwa ndani ya masaa 48 yajayo.
Barcelona italazimika kumlipa Koeman fidia ya Euro milioni 12 kama malipo ya kusitisha mkataba wake kipengele kilichokuwa kwenye mkataba wake.
Klabu hiyo ilitaka kumpa Xavi mkataba wa kuinoa Barcelona mwaka jana lakini alikataa kuwa hakuwa tayari kwa kipindi hicho,lakini katika mahojiano ya hivi karibuni alisema kuwa yupo tayari kuifundisha klabu yoyote duniani kwasasa.