Home Soka Yanga Kuanza Mazoezi Leo

Yanga Kuanza Mazoezi Leo

by Sports Leo
0 comments

Yanga inatarajia kuanza mazoezi yake leo (Mei 27, 2020) chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa ambapo Mazoezi yatafanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar Es Salaam.

Mastaa wa Klabu ya Yanga Haruna Niyonzima(Kushoto) pamoja na Yikpe Gnamien na David Molinga wakiwa wanasubiria kufanyiwa vipimo hapo jana kujiandaa na kuanza rasmi kwa Mazoezi.

Mkwasa amesema atayatumia mazoezi ya leo kuangalia kama wachezaji walikuwa wanatekeleza program waliyopewa na kocha mkuu Luc Eymael ambapo kila mchezaji aliandaliwa aina ya mazoezi ya kufanya pamoja na mlo.

“Wachezaji wote wako vizuri, tutaanza mazoezi rasmi kwa kuanza kutafuta basic endurance na ball work kidogo kwa sababu tumepata program ya kocha mkuu na tutaifanyia kazi”.

banner

“Kwenye mazoezi kuna vitu lazima tuvizingatie (fitness, technic, tactic na phycology) naamini fitness itakuwepo lakini hatuwezi kuanza mazoezi kwa speed kubwa tutaanza taratibu”.

Jana wachezaji wote wa Yanga walikutana na uongozi pamoja na jopo la madaktari kwa ajili ya kupimwa afya na kupewa taratibu za kujikinga dhidi ya Corona wakiwa mazoezini.

Cc:Jamila Kassim

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited