Klabu ya Yanga sc imepanga kukabidhiwa kombe la ubingwa wa ligi kuu wa 30 msimu huu na wadhamini wa ligi kuu bara benki ya Nbc siku ya Jumamosi Mei 25 katika mchezo wa ligi kuu nchini dhidi ya Tabora United utakaofanyika siku ya Jumamosi Mei 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Meneja wa Idara ya habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ally Kamwe amesema kuwa baada ya mchezo huo watagawiwa kombe hilo ambapo kutakua na sherehe kubwa za kushangilia ubingwa huo kuanzia uwanjani hapo kwa burudani za kila aina.
“Mchezo wa tarehe 25 Mei 2024 dhidi ya Tabora United, Young Africans SC tutakabidhiwa Ubingwa wetu na wadhamini wetu NBC, mechi hiyo itachezwa katika Uwanja wa Mkapa”.
“Siku nzima Wananchi tunapaswa kutamba na kuvimba, mageti yatafunguliwa saa tano asubuhi. Kutakuwepo na burudani kutoka kwa wasanii wakubwa kuanzia saa tano” Ofisa habari Yanga Ali Kamwe.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc mpaka sasa katika ligi kuu nchini imefikisha alama 71 ambazo zinawafanya kuwa mabingwa kwa mara ya 30 katika historia ya klabu hiyo huku wakiwa wamesalia na michezo mitatu ya ligi kuu kumaliza msimu na sasa watakua wamechukua taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.