Home Soka Yanga Yahamia kwa Migne

Yanga Yahamia kwa Migne

by Sports Leo
0 comments

Inadaiwa kwamba klabu ya Yanga sc sasa inaisaka saini ya aliyekua kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya ‘harambee stars’ baada ya kushindwana na kocha Hurbet Velud iliyokua inamuwinda hapo awali.

Kocha huyo ambaye anaifundisha timu ya taifa ya sudan kwa sasa ameshindwana na Yanga sc baada ya kuhitaji mshahara wa takribani milioni 50 kwa mwezi jambo ambalo wanajangwani hao wameshindwa kulitimiza.

Sasa baada ya kumgekia Migne ambaye kwa sasa hana timu baada ya kuachana na timu ya taifa ya Equetorial Guinnea kutokana na changamoto za janga la Corona.

banner

Taarifa zaidi zinadai kocha huyo ambaye familia yake inaishi nchini Kenya anaweza kutua nchini siku yeyote kuungana na kocha Juma Mwambusi huku rekodi ya kuipeleka Kenya katika michuano ya Afcon nchini Misri ikiwa imembeba kupata kibarua jangwani.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited