Home Soka Yanga Yatua,Mapokezi Yadoda

Yanga Yatua,Mapokezi Yadoda

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Yanga sc imewasil jijini mwanza asubuhi ya leo kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya ligi kuu dhidi ya Mbao fc,Alliance na ule wa kimataifa dhidi ya Pyramids Fc.

Yanga imewasili na kikosi kamili isipokuwa wachezaji wawili waliopo na timu ya taifa nchini Sudan na kupokelewa na idadi ndogo ya mashabiki kinyume na ilivyotarajiwa na watu wengi hasa baada ya umoja wa matawi ya klabu hiyo jijini humo kuahidi mapokezi makubwa.

Abdulaziz Makame na Golikipa Metacha Mnata waliopo katika kambi ya timu ya taifa watajiunga na timu hiyo kesho baada ya kurejea kutoka Sudan walipokwenda kucheza mchezo wa kimataifa dhidi ya nchi hiyo kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya Chan.

banner

Kocha Mwinyi Zahera ameahidi kufanya vizuri katika mechi hizo baada ya wachezaji wengi kuwa fiti kutumika japo hatakuwepo katika benchi la ufundi katika mechi dhidi ya Mbao akimalizia adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited