Home Soka Yanga,Zesco Hakuna Mbabe

Yanga,Zesco Hakuna Mbabe

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Yanga sc imeshindwa kuonyesha ubabe katika uwanja wa nyumbani baada ya kutoa sare ya 1-1 dhidi ya Zesco united mchezo wa  kwanza ya kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika.

Yanga itabidi wajilaumu wenyewe baada ya kukosa nafasi kadhaa za wazi za kufunga magoli huku wakifanikiwa kupata bao dakika ya 25 kupitia kwa Patrick Sibomana kwa mkwaju wa penati bao lililodumu mpaka mapumziko.

Thabani Skala Kamusoko ndie aliefanikiwa kuwalaza na viatu Yanga baada ya kusawazisha goli dakika ya 94 kufuatia kupiga shuti kali baada ya kutengewa mpira ambao ulimgonga beki Ally Ally na kumuacha kipa Metacha Mnata akiwa hana la kufanya.

banner

Mchezo wa marudiano utafanyika Zambia baada ya wiki mbili na Yanga wanapaswa kushinda ama kutoa sare ya mabao kuanzia mawili ili kufuzu hatua ya makundi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited