Klabu za Namungo na Kmc zinawinda saini ya aliyekua kocha wa zamani wa klabu ya Yanga sc Mwinyi Zahera ili kuzinoa kwa msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara.
Zahera ambaye toka atimuliwe na Yanga sc amekua hana timu ya kufundisha japo muda mwingi amekua akiishi hapa nchini licha ya kuendelea na kibarua chake cha ukocha msaidizi timu ya taifa ya Drc Kongo.
Namungo inatarajia kumkosa kocha wake Hitimana Thierry ambaye anaelekea kujiunga na klabu ya Yanga huku Kmc inatafuta kocha mpya ili kujipanga zaidi baada ya kuwa na matokeo yasiyiridhisha tangu aondoka kocha Jackson Mayanja ambaye nafasi yake ilizibwa na Haruna Hererimana.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.