Home Soka Zidane Akomaa na Kante,Pogba

Zidane Akomaa na Kante,Pogba

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa timu ya Real Madrid Zinedine Zidane ameshikilia usajili wa viungo Paul Pogba na Ngolo Kante kuhakikisha wanajiunga na mabingwa wa ulaya kwa mara tatu mfululizo Real Madrid ili kuimarisha eneo la kati la timu hiyo.

Zidane ametuma ofa ya paundi 86milioni kwa Chelsea ili kuwashawishi kumuuza kiungo huyo mwenye mapafu ya mbwa huku akimtoa kiungo mkolombia James Rodriguez kama chambo kuhakikisha dili hilo linafanikiwa mwezi january.

Huku kwa Pogba licha ya dili hilo kushindikana majira ya joto bado kocha huyo anataka kulifanikisha majira ya baridi huku manchester united wakishikiria msimamo wa kutaka dau la paundi 150 milioni ili kumuuza kiungo huyo mfaransa.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited