Home Makala Mastaa 8 Yanga Kuikosa Mtibwa Sugar

Mastaa 8 Yanga Kuikosa Mtibwa Sugar

by Sports Leo
0 comments

Kocha mkuu wa Yanga , Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kitawakosa wachezaji takribani nane kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utahitimisha msimu wa ligi kuu leo Jumatano katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa kumi jioni.

Nabi amesema maandalizi ya kikosi chake yamekamilika lakini kutokana na sababu mbalimbali kama kutumikia adhabu na wengine kuwa majeruhi, wachezaji hao watakosekana huku pia ikidaiwa wengine anawapumzisha kutokana na kuwa na mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Coastal Union Julai 2.

Aidha ameongezea wanatarajia mchezo wenye ushindani kwani wanafahamu Mtibwa Sugar wanahitaji ushindi ili kujihakikishia kubaki ligi kuu na wao hawatapenda kupoteza mchezo wa mwisho baada ya kufanikiwa kucheza msimu mzima bila ya kupoteza ili kulinda rekodi yao.

banner

Tayari Yanga sc ni mabingwa wa ligi kuu nchini huku Mtibwa wakipambana ili kusalia katika ligi kuu kutokana na kuwa katika hatari ya kushuka daraja.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited