Home Makala Aziz Ki Alamba Tuzo Oktoba

Aziz Ki Alamba Tuzo Oktoba

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Stephane Aziz Ki leo ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi wa klabu yake inayodhaminiwa na shirika la bima la taifa nchini(NIC) baada ya kuwashinda Dickson Job na Maxi Nzengeli.

Ki amewashinda mastaa hao ambao aliingia nao fainali na kupata fursa ya kupigiwa kura na mashabiki wa klabu hiyo kupitia njia ya mtandao(Yanga sc Applications) ambayo ndio njia rasmi ya kupiga kura hizo.

Kutokana na ushindi huo Ki anapewa zawadi ya kiasi cha pesa za kitanzania shilingi millioni nne ambazo zitatolewa na wadhamini wa tuzo hizo ambao ni Shirika la Bima nchini (NIC).

banner

Tuzo hizo ni mara kwanza kutolewa tangu klabu hiyo iingie katika udhamini na kampuni hiyo kwa muda miaka mitatu kuanzia mwaka huu mpaka mwaka 2026.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited