Home Soka Azam Fc Full Mziki

Azam Fc Full Mziki

by Sports Leo
0 comments

Mastaa wa  Azam Fc waliokua katika timu za taifa wamerejea kambini baada ya kumalizika kwa kalenda ya Fifa za michuano ya kufuzu fainali za kombe la Dunia mwaka 2026 zitakazofanyika nchini Marekani,Canada na Mexico.

Mastaa waliojiunga na kambi ya mazoezi ni Feisal Salum, Sospeter Bajana, Lusajo Mwaikenda pamoja na Abdul Suleiman Sopu ambao walikua na timu ya taifa ya Tanzania katika michezo miwili ya kuwania kufuzu fainali hizo ambapo Stars ilicheza dhidi ya Niger na kushinda 1-0 huku ikipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Morroco.

Azam Fc imebakiwa na michuano miwili pekee ya ligi na kombe la shirikisho ambapo mastaa hao wameendelea na mazoezi ili kujiandaa na michuano hiyo ambapo mchezo ujao ambao inatarajiwa kuikaribisha Mtibwa Sugar siku ya ijumaa Novemba 24.

banner

Azam Fc ambayo ilifanya usajili wa nguvu katika klabu zinazoshiriki ligi kuu nchini mpaka sasa ipo katika nafasi ya pili ikiwa na alama 19 katika michezo tisa ya ligi kuu nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited