Home Soka Kipre Jr Kutua Algeria

Kipre Jr Kutua Algeria

by Sports Leo
0 comments

Mazungumzo baina ya klabu ya Azam Fc,wawakilishi wa mchezaji Kipre Junior na klabu ya Usm Algers yanaendelea ili kukamilisha dili la mchezaji Kipre Jr kujiunga na klabu ya Usm Algers kutoka Azam Fc ambapo klabu yake itavuna zaidi ya milioni mia sita.

Mabosi wa Usm Algers ambao ni mabingwa wa kombe la Shirikisho mwaka jana wakimfunga Yanga sc wamevutiwa na uwezo wa staa huyo aliyefunga mabao tisa ya ligi kuu na kutoa pasi tisa za mabao msimu huu na wamewasilisha ofa yao kwa klabu yake ambayo iko mbioni kukubaliwa na dili hilo likamilike.

Sababu kubwa ya Azam Fc kukubali kumuuza staa huyo ni baada ya kujaribu kumuomba aongeze mkataba ambapo aligoma huku akiwa amesalia na mkataba wa mwaka mmoja pekee huku kukiwa na taarifa za kishushushu kuwa Yanga sc wanamnyemelea staa huyo.

banner

Katika makubaliano ya kumuuza staa huyo Azam Fc wameweka kipengele cha kujulishwa mapema kama mchezaji huyo ana nia ya kuondoka klabuni humo ikiwa ni njia ya kuzuia asije kurubuniwa akarudi katika timu za Simba sc na Yanga sc kwa mlango wa nyuma.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited