Home Soka Manyika Amrithi Pondamali Yanga

Manyika Amrithi Pondamali Yanga

by Sports Leo
0 comments

Kipa wa zamani wa klabu ya Yanga sc Peter Manyika ameteuliwa kuwa kocha wa makipa wa timu hiyo kuchukua nafasi ya Juma Pondamali aliyefungashiwa virago klabuni hapo.

Manyika aliyeidakia pia mtibwa sugar ataungana na kocha mkuu Mwinyi Zahera na kocha msaidizi Noel Mwandila ili kusukuma gurudumu la timu hiyo inayojiandaa na ligi kuu na michuano ya kombe la klabu bingwa barani afrika.

Awali ilisemekana nafasi ya Pondamali ingerithiwa na Razack Siwa lakini Manyika mpaka sasa ndie kocha wa makipa wa klabu hiyo akijiandaa kuwaongezea makali makipa wapya Farouk Shikalo na Metacha Mnata pamoja na kipa wa zamani Klaus Kindoki.

banner

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited