Hatimaye kwa mara ya kwanza kwenye historia ya soka barani Afrika la Shirikisho la soka (caf) limepanga kufanya droo ya michuano ya ligi ya mabingwa afrika (CAFCL) na kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kwa msimu wa 2025/2026 ambapo itafanyika jijini Dar es Salaam Tanzania.
Droo hiyo ya hatua ya awali ya michuano hiyo itafanyika Jumamosi hii ya agosti 09 kwenye studio za Azam Media ambaye ni mshirika wa CAF kwa ukanda wa Afrika Mashariki, ukanda ambao unaendelea kuonyesha ukuaji mkubwa wa watazamaji wwa michuano hiyo ya CAFCL na CAFCC.
Katika michuano hiyo msimu huu nchi ya Tanzania itawakilishwa na mabingwa wa ligi kuu nchini Yanga sc na Simba Sc ambao wanashiriki kwenye kombe la Klabu bingwa (CAFCL) huku Azam Fc na Singida Black Stars wakitarajiwa kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye kombe la Shirikisho (CAFCC).
Kwa msimu ujao michezo ya hatua ya awali imepangwa kuanza tarehe 19 Septemba 2025 ambapo timu zitakazofanikiwa kwenda hatua ya pili inayotarajiwa kuanza tarehe 17 Oktoba 2025.
Hatua ya Makundi ya CAFCL na CAFCC itaanza tarehe 21 Novemba 2025 huku hatua ya mtoano ikipangwa kuanza tarehe 13 Machi 2026.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kwa muktadha huo klabu za Simba sc na Yanga sc zote zitaanzia hatua ya awali sambamba na wababe wengine kama Esperance, Rs Berkane na Petro de Luanda ambapo mchanganuo huo ni kwa mujibu wa taratibu na kanuni za Caf.
Klabu za Al Ahly na Mamelodi Sundown ndizo Klabu pekee zitakazoanzia katika raundi ya pili baada ya kukusanya alama nyingi katika renki za Caf huku pia zikifanya vizuri katika michuano hiyo msimu uliopita ambapo zilifika fainali.
Msimu uliopita klabu ya Yanga sc haikufanya vizuri baada ya kuishia hatua ya makundi katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika huku Simba sc ikifanikiwa kufika hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo ilipoteza kwa Rs Berkane.
Tayari klabu hizo zinaendelea na maandalizi kuelekea michuano hiyo ambapo zimeanza kambi baada ya kumaliza usajili wa mastaa kuziba nafasi mbalimbali zenye mapungufu kulingana na ripoti tofauti tofauti za waalimu.
Simba sc imeelekea nchini Misri kwa ajili ya kambi huku Yanga sc ikisalia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ikifanya mazoezi katika uwanja wa Kmc Complex na Augosti 13 itaelekea jijini Kigali Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports Club ya nchini humo.