Senzo Mbatha Mazingiza:Mhandishi Mpya wa Mifumo TRA United

1425530e131d5f2f2ddd17cc2d75830e

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa zamani wa Klabu ya Simba SC mwaka 2018, Senzo Mbatha Mazingiza, anarudi tena Tanzania  safari hii si Msimbazi wala Jangwani, bali atakuwa nahodha mpya wa mageuzi ndani ya TRA United FC, klabu inayomilikiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya uhakika, Awali TRA ilikamilisha hatua za kuinunua rasmi Tabora United FC, timu iliyokuwa ikiwakilisha mkoa wa Tabora katika Ligi Kuu NBC msimu uliopita, na sasa inatarajia kuibadilisha kuwa taasisi bora ya michezo inayosimamiwa kitaalamu na hapo ndipo jina la Senzo linapochomoza kama “mhandisi wa mifumo.”

Senzo Mbatha Mazingiza:Mhandishi Mpya wa Mifumo TRA United-www.sportsleo.co.tz

SENZO MBATHA – MTU WA KAZI SI HADITHI

Senzo Mbatha si jina geni katika anga la soka la Afrika. Ni raia wa Afrika Kusini mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 kwenye uongozi wa klabu barani.
Alianza safari yake ambapo Mbatha amewahi kufanya kazi katika nafasi mbalimbali zenye heshima kubwa, zikiwemo:
Mtendaji Mkuu wa Menza Group (PTY), Meneja Mkuu wa Platinum Stars Football Club, mjumbe wa Kamati ya Tiketi na Usalama ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL), Meneja wa Utawala wa Orlando Pirates, Meneja wa Miradi wa Premier Soccer League (PSL), Naibu Mkurugenzi wa Mashindano wa Kombe la Dunia la FIFA 2010, Mkurugenzi Mtendaji wa Bay United Football Club, na Meneja Mkuu wa University of Pretoria Football Club, miongoni mwa nyadhifa nyingine nyingi.

Kielimu, Mbatha alisoma katika Shule ya Upili ya General Smuts, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Vaal (Vaal University of Technology), na Shule ya Biashara ya Wits (Wits Business School).

Kabla ya kuhamia Simba SC mwaka 2019, akichukua nafasi ya Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo ambapo
ndani ya muda mfupi, Senzo alibadilisha taswira ya Simba akaimarisha mfumo wa kiutawala, akapanga mikakati ya biashara na udhamini, na kuisaidia timu hiyo kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili mfululizo ambapo mashabiki wa Simba bado wanamkumbuka kwa sera yake ya Professionalism First” na nidhamu ya kazi.

KUTOKA MSIMBAZI HADI JANGWANI 

Baada ya kuondoka Simba mwishoni mwa mwaka 2020, Senzo alihamia kwa watani wa jadi Yanga SC – hatua iliyotikisa vichwa vya habari Afrika Mashariki.
Lakini ndani ya Jangwani, alithibitisha ubora wake kwa kusaidia kutengeneza mfumo mpya wa uendeshaji wa kisasa wa klabu, uliosaidia kuzaliwa kwa kile kinachoitwa leo “Yanga ya Kibiashara.”

Senzo Mbatha Mazingiza:Mhandishi Mpya wa Mifumo TRA United-www.sportsleo.co.tz

Alishiriki moja kwa moja kwenye maandalizi ya mabadiliko ya kimuundo, akasaidia kutengeneza mpango wa Yanga SC Company Limited, na kuweka misingi ya uwazi na udhibiti wa mapato,Mafanikio hayo yaliifanya CAF kumtambua kama mmoja wa wataalam wa usimamizi bora wa klabu barani.

BOTSWANA AACHA HISTORIA KUBWA

Baada ya Yanga, Senzo aliendelea na taaluma yake kimataifa kwa kujiunga na Shirikisho la Soka la Botswana (BFA) kama mshauri wa masuala ya utawala na maendeleo ya klabu ambapo akiwa huko, alihusishwa na miradi ya kuboresha kanuni za usajili, udhibiti wa fedha na utawala wa klabu za Ligi Kuu Botswana kisha akarudi nchini kwake lakini kutokana na wasifi huo ndipo TRA ilipomuona kama mtu sahihi wa kuongoza mageuzi ya kiutawala ndani ya klabu yao mpya ya TRA United FC, ambayo inatarajiwa kuwa mfano wa kitaalamu wa timu zinazomilikiwa na taasisi za umma.

TRA UNITED: NDOTO YA KUWA KLABU YA MFANO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imedhamiria kufanya kitu tofauti kuonyesha kuwa hata taasisi za serikali zinaweza kuendesha klabu kwa viwango vya kimataifa,Kwa muda mrefu, changamoto kubwa katika klabu nyingi za Tanzania imekuwa ni kukosa mifumo thabiti ya utawala, uwazi wa mapato na matumizi, pamoja na mikakati ya kibiashara.

Senzo, kwa uzoefu wake katika klabu kongwe kama Simba na Yanga, anatarajiwa kuweka misingi ya:

  • Mfumo wa utawala wenye bodi huru ya usimamizi.

  • Mkakati wa mapato na udhamini wa kibiashara.

  • Mpango wa maendeleo ya vijana na miundombinu ya kisasa.

  • Mfumo wa kidigitali wa taarifa na usimamizi wa wachezaji.

Kwa maneno mengine, TRA United inaweza kuwa klabu ya mfano wa kitaasisi za mpira wa miguu katika nchi za Afrika Mashariki kwa miaka ijayo kama watafanikisha mpango huo.

KWA NINI SENZO NI MTU SAHIHI WA KAZI?

Kwa mujibu wa wachambuzi wa michezo, Senzo ana sifa tatu ambazo ndizo nguzo za mafanikio:

  1. Utaalamu wa kiutawala – anaijua mifumo ya CAF na FIFA kwa undani pamoja na tamaduni za mpira wa Afrika

  2. Uwezo wa kujenga timu za kitaalamu – ameajiri, kuongoza na kufundisha mameneja wengi vijana katika vilabu tofauti pamoja na kujua namna ya kusimamia rasilimali watu katika klabu anayokuwepo.

  3. Uhusiano wa kimataifa – anaheshimika na mashirika ya soka barani, jambo litakachosaidia TRA United kupata ushirikiano wa kiufundi na kuwa na mahusiano mazuri ndani na nje ya nchi,Kwa mtazamo wa wengi, ujio wake unaweza kuanzisha enzi mpya ya usimamizi wa kisasa katika soka la Tanzania.                                                                                                                                                                                                                                                                      HITIMISHO: KUZALIWA KWA NGUVU MPYA YA SOKA LA TAASISI

Kama mambo yataenda kama yanavyopangwa, ujio wa Senzo Mbatha ndani ya TRA United utakuwa mfano halisi wa jinsi soka la Tanzania linavyobadilika.
Kutoka katika klabu binafsi hadi zile zinazomilikiwa na taasisi sasa uwajibikaji, uwazi na ufanisi vinakuwa nguzo kuu.
Senzo anarejea si kama meneja tu, bali kama mjenzi wa mifumo. Na kama alivyofanya Msimbazi na Jangwani, safari hii anakuja TRA  kuandika ukurasa mpya wa historia.

Leave a Reply

Enable Notifications OK No thanks