Home Soka Kalengo ndo Basi tena

Kalengo ndo Basi tena

by Sports Leo
0 comments

Ni kama hana bahati kwani licha ya kushindwa kucheza mara kadhaa kutokana na kuandamwa na  majeraha straika Mzambia wa Yanga Mybin Kalengo amevunjika mguu na kulazimika kupelekwa hospitali haraka.

Nyota ambaye yuko katika kambi ya klabu hiyo jijini Mwanza wakijiandaa na mchezo dhidi ya Pyramids fc ya Misri aliumia wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba ya jijini Mwanza na kulazimika kukimbizwa hospitali ya Bugando jijini humo.

Staa huyo kwa mujibu wa Afisa habari wa klabu hiyo yuko njiani kuja Dar ili kupatiwa matibabu katika hospitali ya muhimbili na ataukosa mchezo huo gumzo nchini.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited