Home Makala Kocha Ataka Wachezaji Wamuige Samatta

Kocha Ataka Wachezaji Wamuige Samatta

by Dennis Msotwa
0 comments

Kocha msaidizi wa Mtibwa Sugar ,Patrick Mwangata amewaasa wachezaji nchini kumuiga nahodha wa Taifa Stars,Mbwana Samatta katika suala la nidhamu na uvumilivu pale wanapopata maisha ya soka nje ya nchi.

Mwangata alisema kuwa wachezaji wengi wa kibongo hawana uvumilivu na nidhamu ya soka na ndiyo maana wengi wao hufanya majaribio nje ya nchi na kushindwa.

Aliongeza kwa kusema kama Samatta asingelikuwa na uvumilivu na nidhamu basi asingelifika hapo alipo na kutokana na kufanya hayo ametutoa kimasomaso hivyo ni muhimu nyota wetu wakajifunza kutoka kwake na kutambua kuwa ili kufika mbali wanahitaji nidhamu ya kutosha na uvumilivu.

banner

“taifa letu linahitaji nyota wengi zaidi ambao wataenda kucheza katika klabu kubwa barani Ulaya na kwingineko duniani ili kuwa na timu ya Taifa imara ambayo inaweza kupambana”alisema Mwangata.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited