Home Makala Job Afungiwa Mechi 3

Job Afungiwa Mechi 3

by Sports Leo
0 comments

Beki tegemezi wa klabu ya Yanga sc Dickson Job amefungiwa na shirikisho la soka nchini kupitia kamati ya tathmini ya michezo ya bodi ya ligi kuu nchini kwa kosa la kumkanyaga kiungo wa Mbeya city Richardson Ng’odya wakati wa mchezo wa ligi kuu uliofanyika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo ambao uliisha kwa suluhu Job alimkanyaga Ng’odya kwenye mbavu wakiwa katika harakati za kugombania mpira na mwamuzi alisimamisha mpira na adhabu ya faulo ikatolewa na ndipo kamati hiyo ikajiridhisha na kuamua kutoa adhabu hiyo kwa mujibu wa kanuni ya udhibiti kwa klabu 41:5(5.3).

Kutokana na adhabu hiyo Job atakosa michezo mitatu ambayo itakua dhidi ya Biashara United mchezo wa kombe la shirikisho kisha atakosa mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar na pia mchezo wa nyumbani dhidi ya Kagera Sugar.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited