Home Soka Arajiga Alamba Tuzo

Arajiga Alamba Tuzo

by Sports Leo
0 comments

Refa Ahmed Arajiga amefanikiwa kushinda tuzo ya mwamuzi bora katika tuzo zilizotolewa jana usiku na Baraza la Michezo Tanzania kutokana na kuonyesha kiwango bora zaidi katika michezo mikubwa nchini Tanzania.

Arajiga mara nyingi huamua michezo yenye uzito mkubwa zaidi nchini ikiwemo mechi baina ya Simba sc na Yanga sc ambayo Simba sc alifungwa 5-1 na hata aliyofungwa 2-0 mara ya mwisho April 20 kocha huyo aliamua mchezo huo.

banner

Arajiga mbali na ligi kuu nchini pia ana beji ya Fifa na tayari shirikisho la soka barani Afrika (Caf) linamtumia katika baadhi ya michezo ya kalenda ya Fifa ya kimataifa ambapo Juni 6 alichezesha mchezo baina ya Malawi dhidi ya Sao tome huku pia akichezesha michezo ya All African Games nchini Ghana kuanzia machi 8 mpka 23 mwaka huu.

Pia kocha huyo msimu huu ameweka rekodi ya kuchezesha michuano ya kombe la Shirikisho la Crdb baina ya Yanga sc dhidi ya Azam Fc visiwani Zanzibar ambapo Yanga sc waliibuka mabingwa kwa penati 6-5 huku ikilazimika kupigwa mpaka penati tisa kwa kila upande.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited