Msafara wa kikosi cha timu ya Azam fc umewasili salama nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo wa pili wa hatua za awali za michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya APR Fc ya nchini humo.
Kikosi cha Azam Fc kimewasili nchini humo siku ya alhamis na mapema leo ijumaa kimeanza mazoezi kuikabili klabu hiyo inayomilikiwa na jeshi la nchi hiyo.
Azam Fc itakua na kibarua kikubwa cha kulinda ushindi wa 1-0 ilioupata dhidi ya timu katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo wa kwanza Azam Fc ilipata bao hilo kwa penati iliyopigwa na Jhonier Blanco baada ya Feisal Salum kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Azam Fc inapaswa kupata sare ya aina yeyote ile ama isifungwe bao lolote ili kujiweka katika uhakika wa kufuzu hatua inayofuatia.