Home Soka Baleke Aanza Mazoezi Yanga Sc

Baleke Aanza Mazoezi Yanga Sc

by Sports Leo
0 comments

Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba Sc, Jean Othos Baleke amejiunga na kambi ya mazoezi ya klabu ya Yanga sc  licha ya mpaka sasa klabu hiyo kuwa kimya kumtambulisha  kama mchezaji mpya wa klabu hiyo yenye makao yake Jangwani Kariakoo jijini Dar es salaam.

Baleke ameripotiwa kujiunga na Mabingwa hao wa Nchi kwa mkopo wa msimu mzima na anatarajiwa kutangazwa muda mfupi ujao kama mchezaji mpya klabuni hapo akitokea klabu ya Tp Mazembe.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba Sc aliondoka nchini na kwenda kujiunga na klabu ya Al-Ittihad Tripoli ambapo amekaa kwa miezi sita tu kisha kurejea nchini ambapo amefanikiwa kujiunga na Yanga sc kwa mkopo wa msimu mzima.

banner

Baleke atakua na kazi ya ziada kupata nafasi ya kucheza mbele ya Prince Dube,Clement Mzize na Kennedy Musonda ambao pia ni wazuri katika eneo la ushambuliaji klabuni hapo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited