Home Soka Chama Anukia Yanga Sc

Chama Anukia Yanga Sc

by Sports Leo
0 comments

Kiungo Cletous Chama anaweza kujiunga na klabu ya Yanga sc wakati wowote kuanzia sasa baada ya kukubaliana maslahi binafsi na klabu hiyo huku mpaka sasa mazungumzo yake na klabu ya Simba sc yakiwa hayajafikia muafaka wa kuendelea klabuni hapo.

Mpaka sasa licha ya kukubaliana na Yanga sc kuhusu mshahara na dau la usajili bado kiungo mshambuliaji huyo hajasaini akisubiri majibu ya mwisho kutoka Simba sc ambao wana mgawanyiko mkubwa kuhusu kumuongezea mkataba kiungo huyo kutokana na bosi mkubwa wa klabu kuhitaji kusajili damu changa klabuni hapo badala ya kumng’ang’ania staa huyo mkongwe.

Pamoja na bosi huyo kuonyesha kutomhitaji Chama bado bosi mmoja ambaye ni anashughulikia masuala ya timu moja kwa moja anamhitaji mchezaji huyo kuendelea kusalia kikosini humo kwa miaka miwili zaidi japo inakua ngumu kwake kukamilisha dili hilo kutokana na ukweli kwamba yeye haidhinishi pesa za usajili.

banner

Chama msimu huu pamoja na klabu ya Simba sc kutokua na kikosi kizuri amejitahidi kuisaidia timu hiyo akifunga jumla ya mabao 7 na kusaidia upatikanaji wa mabao 6 katika ligi kuu nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited