Home Makala Dabi Sasa Kupigwa Juni 25

Dabi Sasa Kupigwa Juni 25

by Sports Leo
0 comments

Bodi ya ligi kuu nchini imetangaza kuusogeza mbele mchezo wa ligi kuu ya soka ya Nbc nchini baina ya Simba Sc na Yanga Sc mpaka juni 25 mwaka huu kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi mpaka sasa.

Taarifa rasmi kutoka bodi ya ligi imesema kuwa mchezo huo uliokua ufanyike jumapili sasa utapigwa siku hiyo mpya huku tayari klabu ya Yanga sc iliyokua imekaa kucheza mchezo wa juni 15 sasa imekubali na kuthibitisha kucheza mchezo huo.

banner

Yanga sc iligoma kucheza mchezo wa jumapili juni 15 mpaka madai yake manne yasikilizwe ikiwemo kutolewa ripoti ya sababu ya kughairisha mchezo wa machi 8 2025 baina ya timu hizo huku pia ikishinikiza kutaka bodi huru ya ligi kuu na ikiwataka viongozi wa bodi hiyo kujiuzuru.

Kwa upande wa klabu ya Simba Sc yenyewe ilikua tayari kucheza mchezo  jumapili juni 15 na ikisisitiza kuwa haiko tayari kucheza tarehe nyingine mpaka sasa bado haijatoa kauli yeyote mpaka sasa kama itashiriki mchezo huo ama lah.

Mapema jioni ya leo baadhi ya viongozi hao wameonekana wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Samia Suluhu Hassan ikulu Jijini Dodoma ambapo haijaelezwa wazi waliitwa kwa ajili gani japo inaonekana kama maada ilikua ni kuhusu mchezo huo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited