Home Makala Henry Sasii Afungiwa Miezi 6

Henry Sasii Afungiwa Miezi 6

by Sports Leo
0 comments

Mwamuzi Hery Sasii amefungiwa miezi sita kufuatia kushindwa kumudu mchezo wa #Ligi kuu ya Nbc nchini kati ya Simba dhidi ya Singida Black stars kwa kufanya maamuzi mengi yaliyoashiria kushindwa kutafsiri sheria 17 za mpira wa miguu.

Sasii ambaye ni miongoni mwa waamuzi wachache wenye beji ya Fifa amefungiwa na kamati maalumu ya kusimamia bodi ya ligi ambapo adhabu hiyo ni kwa kuzingatia kanuni 42.1(1.1) kuhusu udhibiti wa waamuzi.

Katika mchezo huo namba 220 uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam na Simba sc kupata ushindi wa 1-0 na kuchukua alama tatu muhimu.

banner

Katika mchezo huo moja ya matukio yaliyomponza ni pamoja na kukataa penati mbili za Singida Black Stars baada ya Jonathan Sowah kuangushwa ndani ya eneo la hatari huku pia akishindwa kumpa kadi nyekundu Kelvin Nashon kwa kucheza rafu mara mbili akiwa na kadi ya njano.

Kutokana na adhabu hiyo Sasii anatarajiwa kuzikosa mechi za mizunguko mitatu ya ligi kuu iliyosalia pamoja na kukosa miezi mitatu ya mwanzo baada ya ligi kuu kufunguliwa mwezi Septemba mwanzoni.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited