Aliyewahi kuwa Kocha wa Tabora United Fc Anicet Kiazmak ametua katika timu ya Dodoma Jiji Fc ili kuinoa timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kombe la Shirikisho la Crdb nchini.
Uongozi wa Dodoma umeshafanya maamuzi ya kuachana na Kocha Mecky Maxime aliyekuwa na mkataba wa mwaka mmoja ili kupisha usajili ya Kiazmak ambaye aliifanya Tabora United kuwa timu tishio nchini.
Mpaka sasa Dodoma Jiji Fc na Kocha Anicet Kiazmak raia wa DR. CCongo wameshakubaliana kila kitu na kilichobaki ni kocha huyo kusaini mkataba na kuanza kazi moja kwa moja.
Tayari kocha huyo ameshaanza kupendekeza majina ya wachezaji anaotaka kufanya nao kazi klabuni hapo na tayari klabu hiyo imesajili kiungo mkabaji raia wa Congo Drc Nelson Munganga kuja kuungana na kocha huyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mbali na Munganga aliyekua nae Tabora United pia kuna mastaa kadhaa watatua klabuni hapo ikiwa ni matakwa ya kocha huyo kuisuka timu hiyo iwe ya ushindani mkubwa.