Home Makala Kumekucha Yanga sc Vs Sportspesa

Kumekucha Yanga sc Vs Sportspesa

by Dennis Msotwa
0 comments

Siku chache baada ya klabu ya Yanga sc kutambulisha jezi  mpya kwa ajili ya michuano ya kimataifa zenye nembo ya kampuni ya Hier kifuani mdhamini mkuu wa klabu hiyo Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sportspesa ameibuka na kutangaza kutokubaliana na jambo hilo akidai mkataba umekiukwa.

Kampuni hiyo iliachia taarifa maalumu kwa umma ikisema kwamba ilishirikishwa katika mchakato wa klabu kutafuta nembo ya kukaa kifuani katika mechi ya hatua ya makundi ya kombe la shirikisho kutokana na kanuni na taratibu za Caf ambapo mdhamini anayejihusisha na michezo ya kubashiri haruhusiwi kukaa katika jezi za timu yeyote ambapo waliwashauri watumie nembo ya Visit Tanzania na sio nyingine.

Kwa upande wa Yanga sc mpaka sasa hawajatoa taarifa yeyote kuhusu suala hilo huku kampuni hiyo ikipeleka malalamiko hayo kwenye shirikisho la soka nchini(TFF) na likiwataka Yanga sc kufuta nembo hiyo ya Hier katika jezi hizo kwa muda wa siku tatu.

banner

Yanga sc na kampuni ya Sportspesa waliingia mkataba wa udhamini wa jezi ambapo kampuni ilipewa mamlaka kama mdhamini mkuu kukaa mbele kifuani mwa jezi za klabu hiyo katika vikosi vya wakubwa,wanawake na vijana ambapo mkataba huo una thamani ya Takribani Bilioni 12 za kitanzania kwa miaka mitatu.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited