Home Makala Matola Akiri Singida Black Stars Wagumu

Matola Akiri Singida Black Stars Wagumu

by Sports Leo
0 comments

Kocha msaidizi wa klabu ya Simba Sc Selemani Matola amekiri kuwa timu yake ya Simba Sc itakutana na mchezo mgumu itakapowavaa Singida Black Stars katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini kesho Mei 28 2025 katika uwanja wa Kmc Complex.

Matola amesema hayo mapema hii leo katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.

“Singida Black Stars ni timu ngumu sana ni timu ambayo imewekeza, ina wachezaji wazuri na timu ambayo inasumbua katika ligi Kuu ya NBC ila pamoja na ugumu wao Singida Black Stars lakini sisi Simba SC lazima tupate alama zote tatu.”,Alimalizia kusema Seleman Matola

banner

Pamoja na Matola pia katika mkutano huo kocha  wa Singida Black Stars David Ouma naye alikiri ugumu wa mchezo huo huku akibainisha kwamba wamejipanga kuchukua alama tatu katika mchezo huo.

“Simba Sc watarajie kupata ushindani kama walioupata kwenye mechi ya fainali, sisi tayari tumeshafuzu kushiriki mashindano ya CAF msimu ujao, mechi hizi mbili dhidi ya Simba Sports Club tunataka zitupatie level ya ushindani ya mashindano ya CAF.”,Alisema David Ouma Kocha mkuu wa Singida Black Stars.

Timu hizo zinakabiliwa na michezo miwili ndani ya siku tatu ambapo kesho baada ya mchezo huo kumalizika jijini Dar es Salaam timu hizo zitasafiri mpaka Babati mkoani Manyara kuvaana siku ya Mei 31 katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa mchezo wa nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Crdb.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited