Home Makala Mwamnyeto Apewa Ushauri Kutimkia Kwingine

Mwamnyeto Apewa Ushauri Kutimkia Kwingine

by Sports Leo
0 comments

Meneja wa wachezaji ,Jamal Kisongo amempa ushauri beki wa Coastal Union ya Tanga ,Bakari Mwamnyeto kuwa wakati huu ni kwa yeye kujaribu bahati yake kwingine ili kupata changamoto mpya.

Kisongo alisema kuwa nyota huyo ni mchezaji mzuri na hapaswi kuchezea kiwango chake cha sasa bali akitumie kama fursa ya kutoka alipo na kwenda kwingine kwa ajili ya kutafuta mafanikio zaidi.

“Mwamnyeto ni mchezaji mzuri na anajitambua hivyo anapaswa asichezee fursa zitakazotokea hata kama ni nje ya nchi awe mtulivu kufanya maamuzi sahihi  yatakayomsaidia baadaye”alisema Kisongo

banner

Beki huyo wa timu ta taifa ya Tanzania anahusishwa na klabu ya simba na Yanga lakini bado hajasini kokote na viongozi wake wamesema hivi karibuni kuwa timu inayomtaka ijitokeze na kupeleka ofa japo aliwahi kunukuliwa akisema huenda msimu ujao akacheza katika moja ya klabu zitakazoshiriki ligi ya Mabingwa Afrika.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited