Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga sc Nasredine Nabi amefunguka kuhusu sakata la kuwatimua kambini mastaa wake Saido Ntibazonkiza na Dickson Ambundo huku akijitetea kuwa alichukua uamuzi huo kwa manufaa ya timu kuelekea mchezo wa dhidi ya Simba sc.
Nabi alisema kuwatimua wachezaji hao hakuna suala lingine zaidi ya nidhamu bila kujali kama unahitaji matokeo ama ala pia akisisitiza kuwa hakuna timu inayomtegemea mchezaji mmoja.
“Hakuna timu inayomtegemea mchezaji mmoja hata iwe mchangani, kwenye klabu kubwa na inayojiheshimu kuna utaratibu ambao kila mtu anaujua na kama haufuatwi ni tatizo kwahiyo huwezi kuacha kufuata utaratibu kwa sababu unatafuta matokeo”. amesema Nabi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ameongeza, “Ni kweli hicho kitu kimetokea lakini watu wanapaswa kujua wachezaji hawa hawakuwahi kuwa na tatizo hili la kinidhamu lakini kwa kuzingatia umuhimu wa mchezo na kuhitaji kudumisha utulivu kwenye timu tumelazimika kufanya hivyo, ni wachezaji wenye nidhamu siku zote wamekuwa na nidhamu na kuisaidia timu na wataendelea kuisaidia”.