Kocha wa klabu ya Kaizer chiefs Nasredine Nabi ameonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji Kibu Dennis kujiunga na klabu hiyo msimu ujao wa ligi kuu nchini humo.
Nabi ambaye yupo nchini Tanzania kwa mapumziko baada ya ligi kuu ya nchini Afrika ya kusini kufika mwisho moja ya jambo alilolifanya ni kuzungumza na wawakilishi wa mshambuliaji huyo ambaye mkataba wake umesalia na miezi 12 kuona kama anaweza kumsajili kikosini humo.
Nabi tayari ana uhakika wa kuendelea kuifundisha Kaizer Chiefs msimu ujao na anataka kujenga kikosi imara baada ya kufanikiwa kuwapa kombe la kwanza baada ya miaka kumi kupita ambapo mbali na Kibu pia anaangalia uwezekano wa kumshawishi Feisal Salum kujiunga na klabu hiyo pia.