Home Makala “Naiheshimu Azam Fc” Fadlu Asisitiza

“Naiheshimu Azam Fc” Fadlu Asisitiza

by Dennis Msotwa
0 comments

Kocha Mkuu wa klabu ya Simba Sc Fadlu Davis amesema kuwa ataingia kwa heshima katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini baina ya timu yake na Azam Fc utakaofanyika usiku wa leo katika uwanja wa New Amaan complex Visiwani Zanzibar.

Fadlu amesema kuwa ataingia kwa heshima katika mchezo huo kwa maana Azam Fc ni timu kubwa ikiwa na wachezaji wakubwa ambao wanaweza kufanya lolote uwanjani.

“Naheshimu ni mechi ya Dabi haiwezi kuwa nyepesi, ni mchezo muhimu kwetu sisi sote, tumefanya uchambuzi wetu kabla ya mechi hivyo tutakuja na njia mbadala na nzuri kwetu, Azam ni timu nzuri wana safu nzuri ya ulinzi”.Amesema Fadlu Davis wakati akizungumza na waandishi wa habari.

banner

Simba sc itakutana na wakati mgumu dhidi ya Azam Fc katika mchezo huo kutokana na klabu hiyo kuwa na kiu ya alama tatu ambapo mpaka sasa ina alama nane ikiwa imecheza michezo minne huku Simba Sc ikiwa na alama sita katika michezo miwili ya ligi kuu ya soka ya Nbc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited