Home Makala Nataka Kurudi Yanga-Amis Tambwe

Nataka Kurudi Yanga-Amis Tambwe

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa zamani wa klabu za Simba na Yanga,Amiss Tambwe amefunguka kuwa bado ana ndoto za kurejea Yanga kwa sababu ilimfanyia makubwa katika historia yake ya soka, hivyo itakuwa busara na furaha kwake kama ikitokea akapata nafasi ya kurudi tena na kuitumikia.
Tambwe alidumu Yanga kwa misimu minne na kufunga zaidi ya mabao 50 na kuwa moja ya wachezaji waliovuna mafanikio lakini msimu uliopita alijiunga na Fanja FC ya Oman ambayo nayo alivunja nayo mkataba na kurudi kwao Burundi akiwa mchezaji huru hadi sasa.
“Kusema ukweli bado nina mapenzi na Klabu ya Yanga, timu iliyobadilisha maisha yangu na kunipa historia kubwa, hivyo natamani nirudi tena na nicheze pale hadi nitakapostaafu japo watu wanasema niache soka umri wangu umekwenda,jambo ambalo siyo kweli kwani mimi nina miaka minne zaidi ya kucheza na ndiyo maana nasema natamani kurudi Yanga,” alisema Tambwe.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited