Home Makala PSG Kuugawa Ubingwa

PSG Kuugawa Ubingwa

by Sports Leo
0 comments

Baada ya PSG kutangazwa kuwa ni mabingwa wa ligi kuu Ufaransa ‘Ligue 1’na  kufahamika kuwa ligi hiyo haiwezi kuendelea tena kwa msimu huu, beki ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo, Thiago Silva ameugawa ubingwa huo kwa madaktari dunia nzima.

Kutokana na madhara ya virusi vya Corona ambavyo vimeenea dunia nzima ,Ufaransa wao wametangaza kuwa ligi hiyo imefutwa kwa kuwa serikali ya nchi hiyo imesema kuwa michezo itaruhusiwa kuendelea mwezi Septemba mwaka huu.

Beki huyo amesema kuwa ubingwa huo ni kwa ajili ya madaktari wote ambao wanapambana na virusi vya Corona duniani kote kwa kuwa wanafanya kazi ngumu sana na hatari.

banner

“Hakika nisingeweza kufika hapa kama siyo sapoti ya familia lakini hakika ubingwa huu ni maalum kwa ajili ya madaktari wote duniani ambao wanapambana na virusi vya Corona,” aliandika beki huyo raia wa Brazil katika akaunti yake ya Instagram.

Silva aliongeza kwa kumshukuru Mungu kwa kutwaa ubingwa wa saba katika miaka nane aliyokaa Ligue 1.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited