Home Makala Simba sc Basi Tena

Simba sc Basi Tena

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc ni kama imekata tamaa ya kutwaa taji la ligi kuu nchini baada ya kuruhusu suluhu katika mchezo wa ligi kuu nchini dhidi ya Polisi Tanzania uliofanyika katika uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Katika mchezo ambao kocha Pablo Franco aliwapumzisha baadhi ya mastaa wa kikosi cha kwanza akiwemo beki Henock Inonga na Mohamed Hussein pamoja na kipa Aishi Manula na mastaa wengine kama Pape Osmane Sakho alimanusuru timu zote zipate mabao kama zingekua makini baada ya kukosa nafasi kadhaa za kufunga huku Polisi Tanzania wakimiliki eneo la kiungo kwa muda mrefu.

Kitendo cha kocha Pablo kuwapumzisha mastaa wake wa kikosi cha kwanza kimetafasiriwa kama kukata tamaa kuhusu ubingwa wa ligi kuu ambapo Yanga sc inaongoza kwa alama nane ambapo sasa Simba sc ni kama imeelekeza silaha zake katika mchezo dhidi ya Orlando Pirates hatua ya robo fainali utakaofanyika nchini Aprili 17.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited