Home Makala Simba sc Yaishusha Azam Fc

Simba sc Yaishusha Azam Fc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuishusha Azam Fc katika msimamo wa ligi kuu nchini baada ya kuifunga Kmc mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza.

John Bocco alianza kuiandika Simba sc bao la kwanza akiunganisha pasi ya Shomari Kapombe dakika ya 16 ambapo bao hilo lilisawazishwa na Sadala Lipangile dakika ya 52 lakini dakika tatu baadae Augustine Okrah aliiipatia Simba sc bao la pili baada ya mabeki wa Kmc kuzembea kuokoa mpira uliokua unazagaa langoni.

Pamoja na jitihada za golikipa David Kisu Mapigano kuokoa baadhi ya michomo lakini dakika ya 73 Henock Inonga alifanikiwa kuwapatia Simba sc bao la tatu kwa kichwa na mpaka mchezo unafikia tamati Kmc iliangusha alama zote tatu katika mchezo huo.

banner

Simba sc baada ya kupata alama hizo tatu sasa imefikisha alama 41 ikiwa katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu nchini huku Azam Fc ikishuka mpaka nafasi ya tatu na alama 37 na Yanga sc ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo maarufu nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited