Klabu ya Simba Sc imefanikiwa kuibuka na ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex mwenge jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la Steven Mukwala dakika ya 17 ya mchezo liliwahakikishia Simba Sc alama tatu katika mchezo huo na kufikisha alama 77 katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini.
Kagera Sugar hawakuwa na cha kupoteza katika mchezo huo kutokana na kuwa wameshashuka daraja na msimu ujao watashiriki ligi daraja la kwanza.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba sc ilitumia wachezaji wengi ambao hawaanzi mara kwa mara katika kikosi cha kwanza ili kutunza nguvu kwa ajili ya mchezo wa jumatano dhidi ya Yanga sc ambao Simba sc wanapaswa kushinda ili kutwaa ubingwa wa ligi kuu ambao wana takribani miaka mitatu hawajachukua.