Wadau wengi wa soka nchini wamebaki midomo wazi kufuatia uteuzi wa kikosi cha Timu ya wakubwa ya Tanzania(Taifa Stars) baada ya majina makubwa mawili kutojumuishwa katika kikosi hicho ambao ni Shomari Kapombe na Mohamed Hussein.
Mastaa hao hawamo katika kikosi hicho kilichoitwa kwa mara ya kwanza na kocha Adel Amrouche huku pia kikiwa na mastaa watatu tu kutoka katika klabu ya Simba sc ambao wawili ni makipa Aishi Manula na Beno Kakolanya pamoja na kiungo Mzamiru Yassin.
Kwa Upande wa Yanga sc jumla ya mastaa saba wameitwa huku pia jina la kiungo Feisal Salum likijumuishwa hali iliyowaacha wadau wengi midomo wazi kutokana na kutokucheza kwa mchezaji huyo kwa takribani miezi mitatu sasa.
Pia kukosekana kwa kinda Clement Mzize na kuitwa kwa mastaa wengi wanaocheza nje ya nchi nako pia kumeibua maswali kwa waandishi wa habari na wachambuzi wakihoji kuhusu ufuatiliaji wa viwango vya mastaa hao kujua kuhusu viwango vya kwa wakati husika.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kocha Adel Amrouche ameita majina ya mastaa hao kwa ajili ya kuikabili Uganda katika michezo ya hatua za awali ya michuano ya mataifa ya Afrika (Afcon 2024) itakayofanyika mwakani ambapo kwa mujibu wa shirikisho la soka nchini kocha huyo atasaidiwa na Hemed Morrocco.