Home Makala Stars U20 Yatinga Afcon

Stars U20 Yatinga Afcon

by Sports Leo
0 comments

TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes leo Novemba 30 imetinga hatua ya fainali ya mashindano ya Cecafa kwa mbide baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sudani Kusini.

Mchezo wa leo ambao umechezwa Uwanja wa Black Rhino Academy Karatu ulishuhudia dakika 45 timu zote mbili zikienda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo zikiwa zimetoshana nguvu.

Iliawachukua Ngorongoro Heroes dakika 10 ya kipindi cha pilikupata bao la uongozi kupitia kwa Kassim Haruna aliyepachika bao hilo dakika ya 55 baada ya beki wa Ngorongoro, David Kameta kutoa pasi kati iliyokutana na Kelvin John aliyeachia kichwa kikali  kipa akapangua  ndipo mpira ukamkuta Haruna.

banner

Mchezo wa leo ulikuwa ni wa nguvu nyingi kwa kuwa Sudani Kusini walikuwa wakitumia nguvu nyingi mwanzo mwisho jambo lililosababisha kushuhudia kadi nyekundu kwa beki Wayiluki ambaye alionyeshwa kadi ya kwanza ya njano dakika ya 23 na ya pili dakika ya 87 iliyolazimu kuonyeshwa kadi nyekundu.

Nyota mwingine wa Sudani Kusini aliyeonyeshwa kadi ya njano ni Khamis Atari dakika ya 30 na kwa upande wa Tanzania ni Pascal Msindo dakika ya 34 alionyeshwa kadi ya njano.

Ushindi huo wa Ngorongoro utaikutanisha na Uganda hatua ya fainali inayotarajiwa kuchezwa Desemba 2, Uwanja wa Black Rhino huku timu zote mbili zikiwa zimefanikiwa kufuzu Afcon kwa vijana.

Uganda ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Kenya kwenye nusu fainali ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Black Rhino mapema saa sita mchana.

Habari kwa msaada wa Salehejembe.Blog

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited