Unaweza kuwa msimu wa maajabu kwa klabu ya Tabora United kutokana na kuendelea kukusanya alama katika michezo yake ya ligi kuu baada ya kuifunga Kmc ikiwa nyumbani kwa mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex Jijini Dar es Salaam.
Tabora United ilipata mabao hayo katika dakika ya 41 likifungwa na Yacouba Sogne aliyemalizia pasi nzuri ya Heritier Makambo huku Offen Chikola akifunga bao la pili kwa wageni dakika ya 56 kutokana na Tabora kutengeneza shambumbulio la kushtukiza.
Tabora United sasa imefikisha alama 21 katika nafasi ya tano ya msimamo wa ligi kuu ikicheza michezo 13 mpaka sasa ikiwa nyuma kwa alama saba pekee kutoka kwa Simba sc aliye kileleni mwa msimamo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.